Mtaguso

Kutoka Wikibooks

MTAGUSO

Yesu Kristo aliwakabidhi mitume kumi na wawili uongozi wa Kanisa wakiwa kundi moja lenye mkuu wake, yaani Petro. Vilevile waandamizi wao, yaani maaskofu wote, ni kundi moja na papa wa Roma ndiye mkuu wao. Wakatoliki wanaamini kuwa huyo peke yake, na kundi la maaskofu likiwa pamoja naye na chini yake, ndio wenye mamlaka ya juu katika Kanisa lote. Mamlaka hiyo inatumika kwa namna ya pekee unapofanyika mtaguso mkuu, yaani mkutano maalumu wa maaskofu uliokubaliwa na papa kuwa unawakilisha kundi hilo lote. Mitaguso mingine inaweza kuhusu eneo fulani tu, k.mf. nchi au mkoa.



ORODHA YA MITAGUSO MIKUU KADIRI YA KANISA KATOLIKI

KATIKA MILENIA YA KWANZA ILIFANYIKA MASHARIKI (UTURUKI):

1. Nisea I (mwaka 325)

2. Kostantinopoli I (381)

3. Efeso (431)

4. Kalsedonia (451)

5. Kostantinopoli II (553)

6. Kostantinopoli III (680-681)

7. Nisea II (787)

8. Kostantinopoli IV (869-870)


KATIKA MILENIA YA PILI ILIFANYIKA MAGHARIBI (ITALIA, UFARANSA, UJERUMANI):

9. Laterano I (1123)

10. Laterano II (1139)

11. Laterano III (1179)

12. Laterano IV (1215)

13. Lyon I (1245)

14. Lyon II (1274)

15. Vienne (1311-1312)

16. Kostansa (1414-1418)

17. Firenze (1439-1445)

18. Laterano V (1512-1517)

19. Trento (1545-1563)

20. Vatikano I (1869-1870)

21. Vatikano II (1962-1965)


Waorthodoksi wanakubali mitaguso mikuu ya milenia ya kwanza, au ile ya kwanza tu.