Wafransisko
Mandhari
WAFRANSISKO
Fransisko wa Asizi (1182-1226) alianzisha tapo la kiroho lenye matawi makuu matatu: utawa wa kwanza ndio Ndugu Wadogo, utawa wa pili ndio Mabibi Fukara Waklara, utawa wa tatu ndio Wafransisko Wasekulari. Wa kwanza ni wanaume waseja wanaoishi kijumuia, wa pili ni wanawake waseja wanaoishi kimonaki, wa tatu ni wanaume na wanawake wa kila aina.
Jedwali la matunda bora ya familia ya Kifransisko ni kama ifuatavyo:
Wenyeheri Watakatifu Jumla
Utawa I
181 85 266
Utawa II
27 10 37
Utawa III - Waregulari
45 15 60
Utawa III - Wasekulari
69 55 124
Waliovaa kamba
0 4 4
Jumla
322 169 491
Kati yao, 280 ni wafiadini, 3 mapapa, 14 maaskofu, 4 walimu wa Kanisa.